Spread the love
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  

By Safari Mwadanda

Charo Kazungu almaarufu Tungule agonga tena vichwa vya habari kwa moyo wake wa upendo na ukarimu.
Tungule afufua ndoto ya Florence Idza kutoka Majajani wadi ya mnarani katikati ya makao makuu ya kilifi eneo bunge la kilifi kaskazini kwa kumlipia karo za mwaka mzima mwanafunzi yatima aliyekuwa amekata tamaa na kiu ya masomo. Jamii ya Florence imeshindwa kuzuia furaha yao na kumpigia Dua kwa Allah.
Hata mimi pia najumuika na mamia ya watu kumtakia kila lakheri msichana huyu na pia kuzidi kumuombea Rabbi mwenye kutoa na palipopungua pajazwe maradufu.